Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Temba Amcharukia Mtangazaji wa Redio Aliyemuuliza Kama Anabebwa na Chege!

Ukitaka kujua kama ni kweli Mheshimiwa Temba alipitia jeshini basi muulize swali kama anabebwa na Chege kwenye nyimbo zao. Hicho ndicho kilichomkuta mtangazaji wa kituo cha redio cha Victoria FM ambaye kidogo aikimbie studio baada kumuuliza swali hilo

“Ananibebea wapi wakati mimi nimekuja hapa kwa miguu yangu labda sijakuelewa,” alisema Temba kujibu swali hilo.

“Usicheke, nimeuliza vizuri, ananibebea wapi? Sijaelewa, labda huo ni muonekano wa mtu aliyekwambia maanake kila mtu anafanya kazi kwa taratibu zake hata kwenye ngoma ndo jinsi tunavyofanya/ Kiutaratibu yeye lazima akae kwenye chorus, mimi lazima nifanye verse pia ni lazima nifanye intro na nifanye autro, sasa mtu unabebwa vipi? Hujajua kila mtu anaplay kwenye sehemu yake, yeye ni mwimbaji lazima apige chorus na mimi ni rapper! Kwahiyo kama ngoma ni ya kujibizana lazima twende hivyo,” alisema Temba

Kwa upande wa Chege ambaye amedai kukutana na swali kama hilo siku za hivi karibuni alisema:

Kuna watu nilikuwa nawasikia eti bila 50 Cent hakuna G -Unit, sasa kwa nini iitwe G-Unit? Labla wewe unapenda isiitwe Chege na Temba kwa sababu bila Chege na Temba hakuna Chege na Temba, kwa kifupi hilo sio swali, ni kama umekoroga ndonya.!

Nay wa Mitego: Sijali Kama Najihusisha na Ufreemason, Naangalia Naingizaje Pesa

Rapper Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni alizusha maneno mengi kutokana na video ya wimbo wake ‘Mr Nay’ yenye mambo ya kutisha, amewajibu mashabiki wake kwamba hajali kuhusishwa na ufreemason ilimradi anaingiza pesa anayoitaka. 

Akizungumza na kituo cha redio cha Victoria FM kilichopo mjini Musoma, Nay amesema amekuwa akipokea maswali mengi yakitaka kujua kama anajihusisha na jamii ya siri ya freemason kutokana na matendo yake.

“Mimi sijali kama najihusisha na freemason, naangalia jinsi gani naingiza pesa na huu ndio aina ya muziki wangu na kuna mambo makubwa zaidi yanakuja. Muziki wangu na maisha yangu kama yanahusishwa na freemason lakini ninachojali ni pesa tu,” alisema.

MWANAFUNZI WA KIKE WA SHULE YA MSINGI AKAMATWA AKIBA NDANI YA DALADALA MJINI DSM

Waandishi wa ahabari nao wahakuwa nyuma kufuatilia sakata hilo.
Maofisa Usalama wakimpeleka mtoto huyo kituo cha Polisi ili kuweza kupata maelezo zaidi na kusubiri wazazi wake waende kumtoa.
DAR Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Leo mapema asubuhi tulikutana na kituko cha mtoto ambaye ukiangalia unaweza kukuta anaumri wa miaka 12 alikamatwa akimwibia abiria katika daladala na baadae alikamatwa na maofisa usalama wa Jeshi na kuanza kuhojiwa ndipo alipogundulika anamakosa mengi.
Mwanafunzi huyo wa kike wa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam aliyejulakana kwa jina la Irene alipoanza kupekuliwa na maofisa usalama ilionekana mara ya mwisho kuandika ilikuwa ni Aprili 15, 2014 tokea hapo hajaandika, kumbe huwa anawaaga wazazi anakwenda shule huku akiishia Posta jijini Dar es Salaama akilanda landa na mpaka leo alipodakwa.
Katika mahojiano mafupi yaliyofanywa na maofisa hao, ilibainika kuwa mtoto huyo amekuwa na utoro uliokidhiri jambo ambalo hata alipopigiwa mwalimu mkuu wa shule yao ya msingi anaposoma alikiri hilo na kuongeza kuwa mtoto huyo amekuwa akikataa shule kwa muda mrefu pamoja na kupewa taarifa kwa wazazi wao hawakulifuatilia

Dakika 3 za Wema Sepetu akizungumzia yote yanayosemwa ikiwemo isue ya kuajiriwa na Kajala.

LADY JAY DEE: "MAADUI ZANGU WAMEBADILISHA WIMBO" : SOMA ZAIDI HAPA

Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.

Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.

Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa amekuwa katika uhusiano mpya na kijana aliyemzidi umri, jambo analosema halina ukweli.

Habari hiyo inahusishwa na kile kilichodaiwa kuwa mwanamuziki huyo ameachana na mume wake, Gadner G Habash, ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio Times FM.

Jide ameandika: “Hata kama nimeachana na mume wangu, siyo sababu ya kunihusisha katika uhusiano na mwanamume mwingine yeyote. Habari hii imenivunjia heshima. Nafikiri lengo la uzushi huu ni kumfanya Lady Jaydee aonekane mtu asiyefaa.”

Habari hiyo ilipambwa na picha ambazo alizipiga mwenyewe kwa kutumia simu ya mume wake.

Aliongeza: “Ni vizuri kuzusha vitu ambavyo angalau unavijua, hizi picha zilipigwa kwa simu ya Gadner ambaye mnasema nimeachana naye, hamuoni kama mnawadanganya watu?”

Aliongeza kuwa huenda aliyeanzisha habari hizo ameona zile ambazo zilikuwa zikivuma wakati fulani, zimeshuka chati.

Alihoji: “Je, wimbo Jay Dee mgumba, Jay Dee tasa umeshuka chati ndiyo maana mmeamua kuleta mwingine?”

Hata hivyo, alisema lengo la wanaoanzisha uzushi juu yake ni kumdhoofisha lakini anaamini jinsi alivyoshinda vita ya kwanza, atashinda tena vita ya pili. “Hata kama ndoa yangu haiko sawa, niacheni.

Lakini isiwe sababu ya kuendelea kunichafua kwa maneno ya kizushi. Siyo lazima niandikwe, kwa sababu nilikuwapo kabla ya kuandikwa sana... nitaendelea kuwapo bila kuandikwa.