Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Temba Amcharukia Mtangazaji wa Redio Aliyemuuliza Kama Anabebwa na Chege!

Ukitaka kujua kama ni kweli Mheshimiwa Temba alipitia jeshini basi muulize swali kama anabebwa na Chege kwenye nyimbo zao. Hicho ndicho kilichomkuta mtangazaji wa kituo cha redio cha Victoria FM ambaye kidogo aikimbie studio baada kumuuliza swali hilo

Ananibebea wapi wakati mimi nimekuja hapa kwa miguu yangu labda sijakuelewa,” alisema Temba kujibu swali hilo.

Usicheke, nimeuliza vizuri, ananibebea wapi? Sijaelewa, labda huo ni muonekano wa mtu aliyekwambia maanake kila mtu anafanya kazi kwa taratibu zake hata kwenye ngoma ndo jinsi tunavyofanya/ Kiutaratibu yeye lazima akae kwenye chorus, mimi lazima nifanye verse pia ni lazima nifanye intro na nifanye autro, sasa mtu unabebwa vipi? Hujajua kila mtu anaplay kwenye sehemu yake, yeye ni mwimbaji lazima apige chorus na mimi ni rapper! Kwahiyo kama ngoma ni ya kujibizana lazima twende hivyo,” alisema Temba

Kwa upande wa Chege ambaye amedai kukutana na swali kama hilo siku za hivi karibuni alisema:

Kuna watu nilikuwa nawasikia eti bila 50 Cent hakuna G -Unit, sasa kwa nini iitwe G-Unit? Labla wewe unapenda isiitwe Chege na Temba kwa sababu bila Chege na Temba hakuna Chege na Temba, kwa kifupi hilo sio swali, ni kama umekoroga ndonya.!

Comments