Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

KUMPIGIA KURA SALOME MONYO

habari watanzania!
Salome Monyo ni mshiriki wa Bull-BABES Tanzania,anatuwakilisha wasichana na watanzania wote
Ili aweze kushinda anahitaji kura yako na unaweza kumpigia kura mara nyingi uwezavyo kila siku na kila saa ili aweze kutoka na mpunga wa milioni kumi na mbili ili basi aweze kutimiza ndoto zake  zaidi na zaidi maana ndo anaanza kupambana na maisha 
namna ya kumpigia kura ni klick link ifuatayo
http://kileleland.com/bullbabes/profile1839
ahsanteni sana kwa kumfanya salome kuwa mshindi wetu

nuruyetufoundation

nuruyetu foundation ni shirika lisilo la kiserikali linaloendeshwa na mabinti wawili hapa hapa tanzania,,wakiwa na lengo la kusaidia wanawake na watoto kupata mahitaji muhimu,ila kwa sasa wamejikita zaidi katika zoezi zima la ukusanyaji nguo kwa ajili ya wasiojiweza na wenye uhitaji nazo,hivyo waeza kuwafollow kupitia instagram account yao ya (nuruyetufoundation)ili kupata taarifa zaidi,ahsanten

MJUE MWANAMITINDO ANAE SUMBULIWA NA TATIZO LA NGOZI

WINNIE HARLOW ni mwanamitindo ambae amejinyakulia umaarufu sana baada ya kuwa na muonekano wa tofauti katika ngozi yake,WINNIE
HARLOW ni binti mrembo aliejulikana kuwa na tatizo la ngozi alipokuwa na umri wa miaka MINNE,,na ugonjwa wake wa ngozi unaitwa VITILIGO,,ambao upo sehemu za uso na sehemu zingine za mwilini kwake hali iliyomfan
awe maarafu zaidi,, na kwa sasa ni balozi wa shirika mojawapo huko ispaniola,,AMA KWELI MGUU WA KUTOKA MUNGU KAUOMBEA,,KAZA BUTI WINNIE

RAIS MAGUFULI AAPISHWA KESHO

aliejinyakulia ushindi wa kura nyingi dhidi ya wapinzani wenzake wa vyama tofauti ikiwa ni pamoja na edward ngoyai lowassa, CHADEMA,Hashim rungwe CHAUMMA,,anna mghiraACT UZALENDO,,na wengineo,, kwa jina la JOHN POMBE MAGUFULI kupitia chama cha CCM,,ataapishwa mnamo kesho kama raisi wa JAMHURI YA MUUNGANO  WA TANZANIA KWA AWAMU YA TANO, japokuwa ushindani wake ulikua na malalamiko mengi sana kuwa kura zimeibwa,, mara hakustahili,, ila ndo kashapita na pongezi nyingi kwake,, 

NEW AUDIO:DOGO SCOPE---Chausiku


NEW AUDIO:PIZZO FT BERY K -am back

Mshindi wa miss Tanzania 2014 Sitti mtemvu avua taji la umiss Tanzania na kumpatia mshindi namba tatu ambaye alikuwa ni miss Arusha2014 Lilian Deusi,kwa hiyo miss Tanzania 2014 ni lilian deus

SITTI MTEMVU AVUA TAJI LA UMISS TANZANIA

Mwanafunzi wa shule ya msingi Tembon afariki.baada ya kubakwa na vijana watatu tofauti kisha kumchoma kisu na kumtupia tofali kichwani na kufariki papo hapo na baadae kuitupa maiti kichakani ikiwa uchi wa mnyama

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI TEMBONI. DAR   AFARIKI DUNIA BAADA YA KUBAKWA

Mwanafunzi wa shule ya msingi Temboni Dar es salaam afariki Dunia baada ya kubakwa na vijana watatu na kumchoma kisu papo hapo na baadae kumpiga na tofali la kichwa na kutupa,mwili.wake kichakani ukiwa uchi wa mnyama,na leo ndo amezikwa .pichani wanafunzi wenzake wakiwa wamebeba jeneza kwenda kumzika

MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI TEMBONI AFARIKI DUNIA KWA KUBAKWA

Ajali mbaya ya gari imetokea idaru,,ikiwa ni Gari la abiria Happy Nation likitoka Dar kwenda Arusha,,baada ya gari ndogo lililokuwa,likiendeshwa na baba na mtoto wake akiwa ndani ya gari kuingia chini ya basi la abiria na wote waliokuwa kwenye gari ndogo kufariki dunia papo hapo

AJALI MBAYA YA GARI LATOKEA IDARU

Msanii wa bongo fleva Side Boy aliyetamba na wimbo wa kuwa uyone aliyoimba na Ally Kiba na mwingine Usimdharau usiyemjua ,,na ingine kabla hujafa ujaumbika,,,Amefariki leo katika hospitali ya Nyangao iliyoko Lindi baada ya kugua ugonjwa.wa TB Yamifupa,,Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi,,Amin

MSANII WA BONGO FLEVA ,SIDE BOY AFARIKI DUNIA LEO

Mwanamke mwenye ngozi ya chui aliyewahi kutokea miaka 1834 alikuwa ni mwanadada wa Kiafrika ni miongoni mwa watu waliosafirishwa barani Ulaya kwa utumwa,,,na kabla ya kifo chake alimzaa mtoto wake wa kike aitwae LOUISE aliyemrith mama yake ngozi hiyo ya CHUI

MJUE MWANAMKE WA KWANZA DUNIANI ALIYEZALIWA NA NGOZI YA CHUI

Je wajua!!mji mkuu HONGKONG ndo jina peke la mji pekee DUNIANI unaoweza kulitamka bila kuchezesha ulimi na pia bila mdomo kupepesa???

Watoto waoana huko Dodoma,,,katika mahojiano inasemekana tatizo ni kukosa elimu katika kijiji chao,,awali ya kuwa ni kitu kilichozoeleka mahali hapo..na tayar wameshaanza maisha ya ndoa na kupeana majukumu ambapo kazi kubwa ya bibi harusi ni kuchunga mifugo ya nyumbani ikiwa ni pamoja na ng'ombe

Mnyama wa ajabu aonekana pemba akitokea baharini,,,watu.wanasadiki huenda akawa ni Nyangumi,,ila kwa anavyoonekana hafanani na Nyangumi kabisa,,,

JK AKUTANA NA MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA SHERIA NGOWI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi(kulia)alipokutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam alipomtembelea na kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na tasnia hiyo jana.Rais Jakaya Kikwete akizungumza  na ujumbe wa mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (wa kwanza Kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam jana.Rais Jakaya Kikwete akipitia baadhi ya sample za vitambaa vya nguo vinavyotumiwa na mbunifu wa mavazi wa kimatafaifa Sheria Ngowi (kulia)IKULU Jijini Dar es Salaam jana. Mwenye suti ya bluu kushoto ni Makamu wa Rais wa Sheria Ngowi Brand Bw. Haki Ngowi ambaye pia ni blogger maarufu nchini.
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya kumbukumbu  na Ujumbe wa  Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (wa pili kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Freddy Maro)

Temba Amcharukia Mtangazaji wa Redio Aliyemuuliza Kama Anabebwa na Chege!

Ukitaka kujua kama ni kweli Mheshimiwa Temba alipitia jeshini basi muulize swali kama anabebwa na Chege kwenye nyimbo zao. Hicho ndicho kilichomkuta mtangazaji wa kituo cha redio cha Victoria FM ambaye kidogo aikimbie studio baada kumuuliza swali hilo

Ananibebea wapi wakati mimi nimekuja hapa kwa miguu yangu labda sijakuelewa,” alisema Temba kujibu swali hilo.

Usicheke, nimeuliza vizuri, ananibebea wapi? Sijaelewa, labda huo ni muonekano wa mtu aliyekwambia maanake kila mtu anafanya kazi kwa taratibu zake hata kwenye ngoma ndo jinsi tunavyofanya/ Kiutaratibu yeye lazima akae kwenye chorus, mimi lazima nifanye verse pia ni lazima nifanye intro na nifanye autro, sasa mtu unabebwa vipi? Hujajua kila mtu anaplay kwenye sehemu yake, yeye ni mwimbaji lazima apige chorus na mimi ni rapper! Kwahiyo kama ngoma ni ya kujibizana lazima twende hivyo,” alisema Temba

Kwa upande wa Chege ambaye amedai kukutana na swali kama hilo siku za hivi karibuni alisema:

Kuna watu nilikuwa nawasikia eti bila 50 Cent hakuna G -Unit, sasa kwa nini iitwe G-Unit? Labla wewe unapenda isiitwe Chege na Temba kwa sababu bila Chege na Temba hakuna Chege na Temba, kwa kifupi hilo sio swali, ni kama umekoroga ndonya.!

Nay wa Mitego: Sijali Kama Najihusisha na Ufreemason, Naangalia Naingizaje Pesa

Rapper Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni alizusha maneno mengi kutokana na video ya wimbo wake ‘Mr Nay’ yenye mambo ya kutisha, amewajibu mashabiki wake kwamba hajali kuhusishwa na ufreemason ilimradi anaingiza pesa anayoitaka. 

Akizungumza na kituo cha redio cha Victoria FM kilichopo mjini Musoma, Nay amesema amekuwa akipokea maswali mengi yakitaka kujua kama anajihusisha na jamii ya siri ya freemason kutokana na matendo yake.

“Mimi sijali kama najihusisha na freemason, naangalia jinsi gani naingiza pesa na huu ndio aina ya muziki wangu na kuna mambo makubwa zaidi yanakuja. Muziki wangu na maisha yangu kama yanahusishwa na freemason lakini ninachojali ni pesa tu,” alisema.

MWANAFUNZI WA KIKE WA SHULE YA MSINGI AKAMATWA AKIBA NDANI YA DALADALA MJINI DSM

Waandishi wa ahabari nao wahakuwa nyuma kufuatilia sakata hilo.
Maofisa Usalama wakimpeleka mtoto huyo kituo cha Polisi ili kuweza kupata maelezo zaidi na kusubiri wazazi wake waende kumtoa.
DAR Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Leo mapema asubuhi tulikutana na kituko cha mtoto ambaye ukiangalia unaweza kukuta anaumri wa miaka 12 alikamatwa akimwibia abiria katika daladala na baadae alikamatwa na maofisa usalama wa Jeshi na kuanza kuhojiwa ndipo alipogundulika anamakosa mengi.
Mwanafunzi huyo wa kike wa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam aliyejulakana kwa jina la Irene alipoanza kupekuliwa na maofisa usalama ilionekana mara ya mwisho kuandika ilikuwa ni Aprili 15, 2014 tokea hapo hajaandika, kumbe huwa anawaaga wazazi anakwenda shule huku akiishia Posta jijini Dar es Salaama akilanda landa na mpaka leo alipodakwa.
Katika mahojiano mafupi yaliyofanywa na maofisa hao, ilibainika kuwa mtoto huyo amekuwa na utoro uliokidhiri jambo ambalo hata alipopigiwa mwalimu mkuu wa shule yao ya msingi anaposoma alikiri hilo na kuongeza kuwa mtoto huyo amekuwa akikataa shule kwa muda mrefu pamoja na kupewa taarifa kwa wazazi wao hawakulifuatilia